Tupo Nawe

Kadi nyekundu ya Son Heung-min yafutwa, FA wasema ‘Adhabu ilikuwa kubwa’

Klabu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza imeruhusiwa kumtumia winga wao, Son Heung-min katika mechi  tatu zijazo baada ya Chama cha Soka England (FA) kumfutia kadi nyekundu aliyopewa kwenye mchezo dhidi ya Everton.

Kadi hiyo aliyopewa  Son Jumapili ya wikiendi iliyopita iliibua mjadala kabla ya Spurs kupeleka malalamiko kupinga adhabu hiyo kwa Chama cha Soka England (FA).

Kufuatia tukio hilo, Son sasa ataitumikia timu yake kwa mechi zote zijazo, Ambapo awali alitakiwa kukosa mechi tatu.

Son alimchezea rafu, Kiungo wa Everton, Andre Gomes iliyosababisha kiungo huyo kuteguka kifundo cha mguu.

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW