Mitindo

Kishindo cha Ally Rehmtullah 24 Mei

Mwanamitindo maarufu hapa nchini almaarufu kwa jina la Ally Rehmtullah hivi karibuni anatarajia kuzindua mavazi yake ambayo yanatarajia kujulikana kwa jina la Sex In The Event, linalotarajiwa kufanyika katika hotel ya Kilimanjaro Kempinski

Ally Rehmtullah

 

 

 

Mwanamitindo maarufu hapa nchini almaarufu kwa jina la Ally Rehmtullah hivi karibuni anatarajia kuzindua mavazi yake ambayo yanatarajia kujulikana kwa jina la Sex In The Event, linalotarajiwa kufanyika katika hotel ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar Es Salaam.

 
Akizungumza na Bongo5 Ally Rehmtullah alisema kuwa “hii ni moja kati ya show zinazotarajiwa kuwa tofauti na zote ambazo zimewahi kufanyika hapa nchini kwani lengo langu ni kuwaonesha washabiki wa kazi zangu kuwa naweza kutengeneza mavazi ya aina zote tofauti na ilivyozoeleka kuwa ni mtaalamu wa nguo fupi”

 
Katika onesho hili Rehmtullah anatarajia kuonesha nguo ndefu zaidi, tofauti na ilivyozoeleka kwani jamaa ni mmoja kati ya wabunifu ambao wamekuwa wakiaminika kwa kuwa na kipaji kizuuri cha kutengeneza nguo fupi san asana za wanawake.

 
Rehmtullah anataraja kushirikiana na mbunifu mwingine mpya katika soko la kibongo lakini mkali katika masoko ya nje, hivyo anatarajia kumtambulisha rasmi siku hiyo.

 
Katika Onesho hilo litakalofanyika siku ya Jumamosi ya 24 Mei kutakuwa na burudani toka kwa wasanii akiwepo Enika pamoja na Rogers wa Bongo Star Search.

 
Aliwataja wadhamini walioshiriki katika kuifanikisha Show hiyo ni amoja na Barclyars, Air Uganda, Africa Online, Dollywood na Ugo Domingo.

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents