Uncategorized

Klopp afunguka ushindani wake dhidi Manchester City ‘Hakuna wa kuizuiya City bali ni wao wenyewe’

Meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp amesema licha kuwa kikosi chake kina kilakitu lakini bado hakiwezi kuwa tishio kwa Manchester City.

Liverpool's festive fixtures come thick and fast, with Wolves the first of four games in 14 days

Liverpool imeanza vizuri msimu huu hadi kufikia kuwa na jumla ya pointi 45 kwenye michezo yake 17 iliyocheza kwa kushinda mechi 14 na sare mbili ikiwa ni imara zaidi kuliko miezi 12 iliyopita. Kwa mafanikio hayo vinara hao wa ligi wanajiandaa kuwakabili Wolves siku ya Jumamosi na kutarajiwa kuongoza kwa alama nne mbele ya mabingwa watetezi ManchesterCity kama itaibu na ushindi.

Their current form sees them top the league as they prepare to face Wolves on Friday night

Klopp anaamini kuwa City bado ipo kwenye kiwango chake kilekile walichokionyesha msimu uliyopita mpaka wakatwaa ubingwa wa ligi kuu hivyo kama Liverpool wataendelea na kiwango chake walichonacho hivi sasa basi watakuwa sambamba na Pep Guardiola.

‘’City pekee ndiyo inayoweza kujizuia, huo ndiyo ukweli,’’ Klopp ameyasema hayo siku ya Jumanne. 

Jurgan Klopp ameongeza ‘’Ni lazima tucheze mchezo wetu na kupata pointi nyingi kadri tuwezavyo. Siwezi kusema City kama wanabahati.’’

‘’Sisi sote ni washindani, na ndiyomaana tunapaswa kutafakari kwa kila mchezo tunaocheza na kuhakikisha tunapata matokeo, tunayo nafasi ya kutwaa ubingwa hata sisi, kwasababu tunafahamu kazi kubwa tunayofanya lakini pia nafahamu ugumu uliyopo.’’

This image has an empty alt attribute; its file name is 7676968-6517677-image-m-30_1545337778314.jpg

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents