Michezo

Messi atoa ya moyoni kuhusu Ronaldo ‘Nilitamani abaki La liga, El Classico imekosa ladha’ – Video

Messi atoa ya moyoni kuhusu Ronaldo 'Nilitamani abaki La liga, El Classico imekosa ladha' - Video

Nyota wa Barcelona, Lionel Messi amekiri kwamba alitaka Cristiano Ronaldo abaki katika klabu ya Real Madrid. Ushindani wao ulifikia level ya juu sana kwani takwimu zao zilidhihirisha kwamba wao ndio wafalme wa soka duniani kwa mpaka hivi sasa Messi na Ronaldo ndio wanaongoza ktwaa tuzo ya Ballon d’Or wakiwa wametwa mara 5 kila mmoja.

Upinzani wao ulionyeshwa pia kwani vilabu waliokuwa wakichezea vilikuwa na upinzani mkubwa mno hasa kwenye michezo ya El Clasico, ingawa Ronaldo aliondoka Uhispania msimu wa joto wa 2018 kuhamia Juventus.

Messi anajuta uamuzi wa mpinzani wake na anasema kwamba uwepo wa Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno waliutumia kuongeza viungo kwenye mechi hiyo na kuifanya iwe ni yenye mvuta zaidi.

“Nilitaka aendelee kubakia na Real Madrid,” Messi aliambia RAC1. “Aliongeza ubora katika mechi zao za El Clasico na La Liga.

“Real Madrid itaendelea kupeana changamoto kwa sababu wana wachezaji wazuri sana, lakini tayari nilisema kwamba timu hiyo itahisi kupoteza kwake kwa kile Ronaldo alichoonyesha na kwamba kikosi kitagundua hicho.Lakini wanao wachezaji wengi wanaowaruhusu kupigania kila taji na wana historia nyingi. ”

Licha ya kujinyakulia tuzo nyingi alizochukua wakati wote wa kazi yake, Messi hajutii – haswa mchezo wa nusu fainali wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Liverpool msimu uliopita, wakati waliruhusu wapinzani wao kushinda kwa jumla ya mabao 3-0.

“Jambo la Liverpool lilikuwa kosa letu,” alisema, akimtetea Kocha mkuu Ernesto Valverde, ambaye alipata shinikizo baada ya ushindi huo wa Liverpool ambao haujawahi kudhihirisha kweli. “Ilikuja baada ya tukio la kupoteza dhidi ya Roma, Tuliathirika kisaikolojia baada ya kupoteza dhidi ya Roma ya italia.

“Ilizidi kuwa mbaya na haikuwa kwa sababu ya makosa ya kocha “Klabu iliamua aendelee na nadhani kwa kila mtu ilikuwa furaha kwa sababu tunamuunga mkono na kumpenda, kama Luis Enrique au makocha waliokuja kabla yake.”

Wakati huo huo, Messi, ambaye hivi karibuni alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Wanaume wa FIFA kwa msimu wa 2018-19, na huenda akaweka rekodi ya sita ya Ballon, ambayo itamuweka mbele ya Ronaldo katika suala hilo.

“Haitakuwa fedheha kutoshinda,” alisema. “Tuzo hizi ni nzuri kutambuliwa, lakini kwangu zilikuwa sio kipaumbele, ningefarijika zaidi kutumia mwaka mwingine bila kushinda Ligi ya Mabingwa – imekuwa miaka mitano tangu tumefanya hivyo.”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents