Habari

Mfahamu kikongwe wa miaka 80 ambaye ni fundi wa radio za magari

Mfahamu kikongwe wa miaka 80 ambaye ni fundi wa radio za magari

Bibi mmoja anayetambulika kwa jina la Cecilia Wangari mwenye umri wa miaka 80 amejizoelea umaarufu mkubwa jijini Nairobi nchini Kenya kutokana na kazi zake anazozifanya.

Cecilia akiwa katika harakati za kuibadilisha redio ya mteja

Bibi huyo maarufu kwa jina la ‘Shosh’ ameonekana kuwa tofauti na watu wenye umri kama wake ambao maranyingi huishi majumbani na kuwategemea watoto wao au hata wajukuu kuwalisha lakini kwa Cecilia ni tofauti kabisa.

Cecilia akifungua redio ya gari la mteja

Kwa mujibu wa BBC bibi Cecilia anaduka lake la kuuza, kurekebisha na kuweka upya radio za magari lililo barabara ya Outering mjini Nairobi, huku akiwa mwenye shughuli nyingi kwa wateja kuhitaji huduma yake.

Akizungumza na chombo hicho cha habari bibi Cecilia amesema kuwa amekuwa ni mtu wa kujishukhulisha kwa shukhuli mbalimbali tangu miaka ya 70.

Mimi nilizaliwa Nairobi na nimefanya biashara kadhaa tangu miaka ya sabini na hata nilikuwa na gari langu.

Nilikuwa nimeajiri dereva na kondakta lakini mara nyingi walikuwa wananilaghai wakinidanganya kuwa gari limeharibika ninawapa pesa lakini hawanunui vipuri. Ndipo nikaamua nifanye kazi ambayo nitakuwa naisimamia mimi mwenyewe

Cecilia anaonekana bayana kuwa na ujuzi wa juu kuhusu mambo ya radio za magari kulingana na jinsi anavyoelezea na kushughulikia wateja wake.

Cecilia akikarabati mitambo

Anasema licha ya yeye kutokuwa na kisomo chochote alianza kujifunza taratibu kuanzia mwaka 1991 kukarabati na kufunga radio za magari kwa fundi mmoja mara nyingi kwa kuangalia tu jinsi kazi hiyo ilikuwa ikifanywa.

Fundi aliyenifundisha aliniambia ninunue vifaa vichache tu ambavyo nilitumia kujifunzia hii kazi na tangu wakati huo nimeifanya kazi hii kwa miaka yote hii, ni kazi ninayoifurahia kwa saabu ninaipenda

Kila wakati ninahakikisha kuwa wateja wangu wameridhika na huduma yangu na pia ninawazungumzia kwa njia nzuri ndio wapate kurudi tena

Kazi ni kazi, hakuna kazi ya kufanywa na mwanaume au mwanamke, hata kama ni ya kupaka viatu rangi rangi, ni kazi inayoweza kufanywa na kila mtu, kwa hivyo mtu asichaguae kazi

Bibi Shosh ana vijana kadhaa wanaomsaidia na kazi kwenye duka lake na baadhi yao ni wajukuu wake ambao anasema anataka awasaidie kujimudu kimaisha na waweze kujitegemea siku za usoni. Wateja wengi wanaofika duka la Shosh hutaka huduma yake mwenyewe.

Akihudumia wateja

Anasema siri kuu ambayo imechangia yeye kuwa kwenye biashara hii kwa kipindi kirefu kama hiki na wateja kumpenda ni kuwa mkweli kwa kazi yake na kuwaheshimu wateja.

Anasema biashara hii imemwezesha kujikimu kimaisha. Anawashauri watu wote, wanaume kwa wanawake, wasichana kwa wavulana wasichague kazi.

"Kazi ni kazi, hakuna kazi ya kufanywa na mwanamume au mwanamke," anasema Cecilia

Pia anasema kuwa kufanya kazi kwa uaminifu imekuwa nguzo muhimu kwa biashara kwa kazi yake. Ni lazima kila wakati ahakikishe kuwa ana leseni zote zinazohitajika kwa biashara yake ili kazi yake iweze kuendelea. Licha ya umri wa miaka 80 Cecilia anasema ana ndoto kubwa ya siku za usoni.

Ni lazima nihakikishe kuwa duka langu lina leseni na hata bango lililo nje ya duka na ni lazima nililipie ili kuhakisha kuwa ninafanya biashara bila ya usumbufu wowote

Ningependa siku moja niwe na shule ya kuwafunza vijana kazi hii ya ufundi wa redio. Niwe na shule ambayo mimi mwenyewe nitahakikisha kuwa nimempa mwanafunzi cheti baada ya kuhitimu vizuri

"Kazi ni kazi, hakuna kazi ya kufanywa na mwanamume au mwanamke," anasema Cecilia

Bibi Cecilia ameongeza kuwa kamwe hana mpango wa kuachana na kazi hiyo siku za hivi karibuni hatakama Mungu atambariki kuishi miaka 200.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents