Soka saa 24!

Mhe. Godbless Lema aahidi kujiuzulu Ubunge ‘Chama kitatoa tamko juu ya hili’

Mbunge wa Arusha Mjini kupitia tiketi ya CHADEMA, Mhe. Godbless Lema ametangaza kuwa atajiuzulu nafasi hiyo, endapo Spika wa Bunge, Job Ndugai atathibitisha kuwa Tundu Lissu amelipwa fedha kwa ajili ya matibabu.

Image result for godbless lema
Godbless Lema

Lema amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter, ambapo amesema taarifa iliyotolewa na Spika Ndugai sio ya kweli.

Bunge halijawahi kumlipia Mh Lissu pesa kwa ajili ya matibabu, alichokisema Mh Spika Ndugai ni upotoshaji kwa jamii na Mungu.Chama kitatoa tamko juu ya hili.Spika akiweza kuthibitisha hili,Mimi nitajiuzulu Ubunge,mshahara wa Mbunge sio hisani ya Spika.“ameandika Godbless Lema .

Leo Alhamisi Januari 31, 2019 bungeni jijini Dodoma, Spika Ndugai amesema kuwa hadi mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki, alikuwa amelipwa TSh milioni 207.8 .

Spika Ndugai amesema kuwa Mbunge huyo, Tundu Lissu amekuwa akilalamika kila wakati kuwa Bunge halimjali kitu ambacho hakina ukweli ndani yake.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW