Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Mimi na mke wangu Shamsa hatugombani, nikimkosea najishusha tu – Chidi Mapenzi

Mfanyabiashara, Chidi Mapenzi ambaye ni mume wa ndoa wa muigizaji, Shamsa Ford amefunguka kwa kudai kwamba yeye na mke wake huyo huwa hawafikiagi hatua ya kugombana kwani akigundua amemkwaza mwenzake huwa anajishusha chini na kuomba msamaha.

Chidi amekanusha kwamba penzi lao lipo hatarini kuvunjika huku akidai kwa sasa wapo vizuri na wanafurahia maisha yao.

“Mimi ni mke wangu huwa hatugombani, nikimkwaza lazima niwe chini nitafanyaje,” Chidi Mapenzi alikiambia kipindi cha Shilawadu cha Clouds TV. “Mke wangu nikimkosea huwa anakuwa na hasira lakini baadaye hasira zinaisha na maisha yanaendelea,”

Chidi amesema sio kweli kwamba ndoa yao ilikuwa ivunjike, yote ambayo yalikuwa yanazungumzwa na mitandao ya kijamii kwamba ndoa yao ipo mbioni kuvunjika sio ya kweli.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW