Soka saa 24!

Neymar aumia kwenye mguu ambao ulimuweka nje ya michuano ya kombe la dunia, hofu yatanda kuikosa Man United

Miamba ya soka nchini Ufaransa klabu ya Paris Saint-Germain imethibitisha kuwa mshambuliaji wake raia wa Brazil, Neymar amepata majeraha kwenye kifundo cha mguu ule ule ambao aliwahi kuumia na kumkosesha na michuano ya kombe la Dunia mwaka jana nchini Urusi.

Kuumia kwa nyota huyo kumezua hofu miongoni mwa wapenzi wa soka kuwa huwenda akaukosa mchezo wake wa Champions League dhidi ya Manchester United mwezi ujao.

Mchezaji huyo ghali zaidi duniani ameumia kwenye mchezo wa French Cup dhidi ya timu ya Strasbourg ambapo waliibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2 – 0.

Ingawa meneja wa Strasbourg, Thierry Laurey pamoja na wachezaji wake wawili wanalaumiwa juu ya tukio hilo la Neymar lakini pia aina ya uchezaji wa nyota huyo wa Brazil nayo inatiliwa mashaka.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW