Uncategorized

Hiki ndicho alichosema Mourinho wakati Ronaldo akitwaa Ballon d’Or yake ya kwanza mwaka 2008 akiwa Man United

Kocha mwenye maneno mengi zaidi duniani Mreno Jose Mourinho hakuamini wakati Cristiano Ronaldo akitangazwa kuwa ndiye mchezaji bora wa dunia mwaka 2008 na kukabidhiwa tuzo ya Ballon d’Or.

Ronaldo akikabidhiwa tuzo hiyo baada ya kufanya kazi kubwa kabisa msimu wa mwaka 2007 na kuwashinda wapinzani wake kwa wakati huo kama vile nyota wa Barcelona, Lionel Messi na straika wa Liverpool, Fernando Torres.

Miongoni mwa waandishi wa habari 96 kutoka France Football, 77 walimpigia kura nyota huyo wa Manchester United wakati huo baada ya kufunga jumla ya mabao 42 na kuisaidia United kutwaa taji la Premier League pamoja na Champions League mara mbili.

Ronaldo akiibuka mshindi kwa kuwa na ponti 446 kati ya 480, huku Messi aikishika nafasi ya pili na alama 281 na nafasi ya tatu ikishikiliwa na Torres aliyepata pointi 179.

Kijana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 23 wakati huo akawa Mreno wa watatu kutwaa taji hilo kubwa kabisa baada ya Eusebio na Luis Figo huku ndani ya United akiwa ni George Best, Denis Law na Bobby Charlton.

Na mara baada ya kutwaa tuzo hiyo ya mchezaji bora, Mourinho alikataa kuwa Mreno mwenzake alistahili kuchukua.

“Ronaldo ni mchezaji mzuri lakini siyo bora,” alisema Mourinho mwaka 2008, wakati kijana huyo akitwaa tuzo yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 23.

Cristiano Ronaldo Receiving the European Footballer of the Year Award, Boulogne-Billancourt, Paris, France - 07 Dec 2008

Jose Mourinho ameongeza “Amestahili kuchukua Golden Ball kwasababu timu yake imeshinda ubingwa wa Champions League na Premier League. Lakini kwangu mimi, Ibrahimovic ndiyo bora.”

Mourinho wakati huo alikuwa akiifundisha Inter Milan ambapo Ibrahimovic akiwa anaitumikia timu hiyo ambaye kwa sasa amestaafu kuitumikia timu yake ya taifa ya Sweden.

Ibrahimovic hajawahi kushinda Ballon d’Or mpaka sasa zaidi ya kutwaa ubingwa Champions League.

Huku Mourinho akishinda ubingwa wa Champions League akiwa na Inter mwaka 2009, lakini alikosana na mchezaji huyo kisha akatimkia Barcelona.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents