Habari

Polisi Belarus ruksa kutumia silaha za moto kukabiliana na waandamanaji

Polisi wa Belarus wameruhusiwa kutumia silaha za moto kukabiliana na waandamanaji pale inapolazimika kufanya hivyo huku serikali ya Minsk ikilaani maandamano yenye msimamo mkali dhidi ya serikali.

Polisi wa Belarus wapewa amri ya kutumia silaha za moto wakati wa maandamano.

Vikosi vya usalama viliwakamata watu 713 siku ya Jumapili na kutumia maji ya kuwasha na fimbo kuwatawanya waandamanaji wanaotaka uchaguzi mpya wa urais.

Maelfu ya raia wa Belarus wamekuwa wakiandamana kila mwishoni mwa wiki tangu kuchaguliwa tena kwa Alexander Lukashenko Agosti 9. Kulingana na upinzani wanadai ameshinda uchaguzi huo baada ya kughushi matokeo ya uchaguzi.

Oktoba 2, Umoja wa Ulaya uliweka vikwazo dhidi ya maafisa karibu arobaini wa Belarus wanaodaiwa kuhusika katika udanganyifu wa uchaguzi na ukiukaji wa haki za binadamu.

Kwa kujibu, rais wa Belarusi, ambaye Vladimir Putin ndiye mshirika wake mkuu, alitangaza siku hiyo hiyo kwamba alikuwa ameandika orodha ya watu waliopigwa marufuku kuingia katika nchi yake na aliwarejesha nyumbani mabalozi wake waliokuwa nchini Poland na Lithuania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents