Habari

Serikali yachukua maamuzi kuhusu Meli zilizokamatwa na silaha na dawa za kulevya

Serikali ya Tanzania imechukua maamuzi ya kuzifutia usajili meli mbili za Tanzania zilizokamatwa zikiwa na shehena ya dawa ya kulevya na silaha, huku ikikana kuhusika na mzigo uliokatwa nazo na kuamuru meli hizo kushusha bendera ya Tanzania.

Picha inayohusiana
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan

Maamuzi hayo yametolewa leo Alhamisi Januari 18, 2018 Ikulu Jijini Dar es salaam na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ambapo amesema kuwa meli hizo zilisajiliwa chini ya mamlaka ya usajili wa usafiri wa baharini kinyume na sheria.

Tanzania haihusiki na shehena za silaha wala mdawa ya kulevya yaliyokamatwa ndani ya meli hizo, bali ilitoa usajili wa meli hizo chini ya mamlaka za usajili ambao ni utaratibu wa kawaida wa kimataifa wa kusajili meli duniani, kwa hiyo kufuatia tukio hilo, tumezifutia usajili meli zote mbili, usajili ulitolewa chini ya taasisi ambayo ilishanyimwa kibali cha kusajili meli, na sasa meli zote zimeshusha bendera ya Tanzania ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa”, amesema Mama Samia Suluhu na kufafanua ufutaji wa usajili wa meli hizo.

“Tumefuta usajili wa Meli hizo na kuwataka washushe bendera yetu na wapambane na tatizo hilo wao wenyewe na sisi tupo tayari kutoa ushirikiano wowote pale utakapohitajika,”amesema Mhe Samia Suluhu Hassan.

Mama Samia amezitaja Meli hizo kuwa ni Kaluba yanye usajili Namba IMO 6828753 iliyokamatwa Jamhuri ya Dominika ikiwa na kilo 1600 za dawa za kulevya, na nyingine ni Andromeda yenye namba IMO 7614966 iliyokamwa ikiwa na silaha zilizokuwa zikisafirishwa kwenda Libya kinyume na sheria za kimataifa na Meli zote zilikamatwa mwezi Desemba mwaka jana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents