Shamsa Ford atoboa siri ya mastaa wa kike kufeli katika mahusiano

Msanii wa Filamu Bongo, Shamsa Ford amefunguka sababu ya baadhi ya mstaa hasa wa kike kutodumu katika mahusiano.

Muigizaji huyo amesema mahusiano ya watu maarufu hayadumu kutokana wanaingiza umaarufu wao katika mahusiano yao. Kupitia ukurasa wake Instagram Shamsa ameandika;

“Nimegundua mahusiano mengi ya watu maarufu hayadumu kwa sababu wengine huwa wanaleta Ustar hadi kwenye mahusiano, hata mtu wa kawaida akiwa na uhusiano na mtu maarufu ni mara chache sana kudumu,” amesema.

“Hasa kwa upande wa wanawake huwa tunaamini ustar ndo kila kitu kwa mwanaume kumbe sio, sasa sijui hatuna elimu ya ustar au vipi kwa hapa Bongo, maana ingekuwa ustar shida Beyonce na Jay Z wasingedumu mpaka leo na hawa ndo mastar wa dunia,” amesisitiza.

Soma Pia; Hayawi hayawi, Shamsa Ford aolewa

September 2016 Shamsa Ford alifunga ndoa na mfanyabiashara wa maduka ya nguo Rashidi Saidi a.k.a Chidi Mapenzi.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW