Habari

Video: IGP Sirro asema baada ya upekuzi wabaini gari ni lilelile alilotaja ‘gari ni lilelile halina mashaka’

Mara baada ya kupatikana kwa mfanyabiashara na mdhamini wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ambaye aliripotiwa kutekwa na watu wasio julikana katika Hotel ya kifahari ya Collesium alifajiri wakati anaenda mazoezini siku chache zilizopita, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP  Simon Sirro amesema kuwa baada ya kufanyika kwa upekuzi wa gari lililotelekezwa wamegundua ni lilelile ambalo namba zake amezitaja na hata alivyoangalia vioo kwahiyo hakuna mashaka.

IGP Sirro ameyasema hayo alipofanya mkutano na waandishi wa habari mapema asubuhi ya leo siku ya Jumamosi.

”Nilieleza uwelekeo wa lile gari na nilieleza ufuatilijia tuliofanya mpaka kwenye mipaka yetu na kuona lile gari lilipita tarehe 1 ya mwezi wa tisa mwaka 2018 kwahiyo kweli gari lilikuwa hapa nchini. Usiku wa kuamkia leo majira ya saa 7 karibu na nusu hilo gari limetelekezwa hilo gari lilikuwa pamoja na Mohammed Dewji,” amesema IGP Sirro

Kamanda Sirro ameongeza ”Kwahiyo alipofika pale baada ya kumteremsha kwenye ile gari alitemremka wao wakaondoka lakini walijaribu kwanza kuliunguza lile gari. Kwahiyo kwa maelezo ya Mohammed ‘MO’ alipata mlinzi mmoja akapiga simu kwa wazi wake baadaye ndiyo na sisi tukapata taarifa na Polisi wakawahi kwenye eneo la tukio.”

”Upekuzi umefanyika asubuhi chini ya timu yetu inayohusika na mambo ya matukio, kwenye hiyo gari tumebaini gari ni lilelile ambalo namba zilezile ambazo nimezitaja na ukiangalia hata kwenye vioo ninamba zilezile nilizozitaja kwahiyo gari ni lile halina mashaka.”

”Ndani ya hiyo gari tumekuta silaha nne, silaha hizo kuna AK 47 moja ambayo inarisasi 19 lakini kuna pisto tatu ambazo jumla zinarisasi 16. Kwahiyo kimsingi MO alivyohojiwa amesema walewatu baada ya kumteka walikuwa na wasiwasi sana na walichokuwa wanaomba kwake wanaomba fedha na yeye akachukua simu ya baba yake akawapa namba akawaambia namba hii mkimpigia baba mtazungumza naye lakini wale watu wakachukua namba wakawa wanawasiwasi hawakutaka kuzungumza na baba yake na lugha waliyokuwa wakizungumza ilikuwa ni Kiingereza na Kiswahili kidogo chakubahatisha.”

”Kwahiyo kimsingi upelelezi upo vizuri niwashukuru sana wananchi wa Dar es Salaam ambao wameendelea kutupa taarifa kwasababu mchezo ndiyo unaanza sasa, tunataka kuwaonyesha Tanzania siyo mahala ambapo salama kwa mtu yoyote anayetaka kuja kufanya uhalifu.”

”Nafikiri lile tangazo nililotoa na picha ilivyoonekana basi wakawa na wasiwasi kabisa ya kwamba wamgekamatwa na kweli wangekamatwa, hawakuwa na namna mmiliki wa gari tayari tunajua, dereva tayari tunajua ilibakia tu kufuatilia kujua hiyo gari ipo wapi.”

”Kunakikundi cha watu ambao jeshi la Polisi au vyombo vya ulinzi na usalama na unyeti wake wakipeleleza jambo lolote wao wanaingilia tena wanaingilia sana na wanaingilia kwa kufundisha majeshi yafanyeje kazi na hasa jeshi la Polisi.”

”Niwaombe sana kwamba wasilazimishe kujenga uwadui na majeshi yetu, wasilazimishe kujenga uwadui na jeshi la Polisi wajue haya wanayoyafanya yote kwasababu ya usalama uliyopo. Wajitahidi sana kushirikiana na majeshi yao, wasilazimishe kujenga uwadui na majeshi yetu.”

”Najiuliza unapojenga uwadui na majeshi yako unatumwa na nani, kwafaida ya nani, ili kiwe nini, ? nataka Watanzania hilo mlielewe. Mimi siyo mtu wa siasa ninakwenda kwenye maadili yangu ya kazi, hata siku moja hamjawahi kusikia IGP anazungumza mambo ya siasa.”

”Kunawatu amabao eidha kwakutumwa au kwafaida yake binafsi wanataka nchi yetu isikalike, iyonekane Serikali yetu imeshindwa. Lakini niwaambie hao ndugu zao wanaowatuma hawatapata nafasi.”

”Sisi tupo imara, wananchi wapo imara na ndiyomaana hata unaona wengine mauwaji yalivyokuwa yanafanyika Kibiti watu wetu wanakufa wengine wanasherehekea, wengine wanafurahia sasa niswala la kujiuliza je tupo pamoja nao ?.”

Kwa mujibu wa familia yake, Mo Dewji ambaye ni mfanyabiashara hapa nchini ametekwa na watu wa siyo julikana majira ya saa 11: 35 mpaka saa 11: 40 tarehe 11 Oktoba  2018 Colosseum Hotel Mtaa wa Haile Selasie Oysterbay Dar es salaam .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents