Soka saa 24!

Wagonjwa 250 walioshindwa kulipia matibabu Kenya, watolewa hospitalini

Hospitali kuu Nchini Kenya ya Kenyatta imesema kuwa imewaachilia huru wagonjwa 52 kwenda nyumbani kufuatia madai kwamba walikuwa wanazuiliwa baada ya kushindwa kulipa gharama zao za matibabu.

Taarifa kutoka hospitali hiyo ya kitaifa imesema kuwa zaidi ya wagonjwa 250 wameruhusiwa kuondoka.

Hospitali hiyo imekana madai kwamba baadhi ya wagonjwa walikuwa wamezuiliwa kinyume na matakwa yao, Ni kawaida kwa hospitali nchini Kenya kuwazuilia wagonjwa kuondoka hadi wanapolipa gharama zao za matibabu.

Msemaji wa Hospitali hiyo, Hezekile Gikambi Peter amekana kwamba wagonjwa hao walikuwa wakizuiliwa na kuongezea kuwa wasingezuiliwa kuondoka katika hospitali.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW