”Watanzania wachukue tahadhari kujikinga na mafua makali yanayosababishwa na kirusi kipya CORONA”-Wizara ya Afya

''Hadi sasa Tanzania haina mshukiwa wa ugonjwa huo''

Wizara ya Afya imesema mpaka sasa Tanzania haina mshukiwa wa ugonjwa wa homa ya mafua makali inayosababishwa na kirusi  kipya[CORONA],ambapo wizara imechukua tahadhari kutokana na Tanzania kuwa na muingiliano wa kibiashara na kijamii kati ya China na nchi nyingine kwa Watanzania wanaosafiri kwenda mataifa yaliyoathirika na mlipuko wa ugonjwa huo.

“Dalili za ugonjwa huo ni mafua makali,kuumwa kichwa mwili kuchoka ,kikohozi,kubanwa mbavu,kuathirika mapafu,kupumua kwa shida na hata kifo”

“Watanzania wachukue hatua ya kujikinga na ugonjwa huo kwa kufunika mdomo na pua wakati wa kukohoa,kukaa mbali mtu aliyeathirika na Kirusi hicho hasa kwa wale wanaosafiri mataifa yenye Mlipuko na kuwahi kituo cha afya ukihisi dalili za ugonjwa huo,”Wizara ya Afya

Na Jacquiline Ngoya

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW