DStv Inogilee!

Watu 20 wafariki dunia kwenye ajali ya Treni Misri, wengine ni majeruhi baada ya tanki la mafuta kulipuka

Watu 20 wamekufa na wengine 40 kujeruhiwa baada ya kutokea ajali ya treni katika njia kuu ya treni nchini humo.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la BBC, Tukio hilo limetokea baada ya treni hiyo kugonga kizuizi cha kupunguza kasi, katika kituo kimoja cha treni katikati ya mji.

Ajali hiyo imesababishwa na kulipuka kwa tanki la mafuta la treni hiyo, hali iliyosababisha majengo ya jirani pia kuungua.

chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana, lakini saa chache baadaye, Waziri anayeshughulika na usafiri Hisham Arafat alijiuzulu.

Majeruhi wakisaidiwa

Majeruhi wakisaidiwa

Watu walioshuhudia ajali hiyo wamesema wameona miili kadhaa katika janga baya kukumba nchi hiyo katika siku za hivi karibuni, hususan kwa usafiri wa treni.

Mmoja wa mashuhuda, Ahmed Mahmoud ameliambia shirika la Habari la AFP, kuwa alitoa miili ya watu 20 na kuiweka kwenye gari la wagonjwa, yote ikiwa imechomeka.

Aidha amesema kawaida treni likikaribia kituoni huja kwa mwendo wa taratibu, lakini siku hiyo lilikuwa katika kasi.

Awali vyombo vya habari vya nchi hiyo viliripoti kwamba watu waliofariki ni 25 huku wengine 50 wakiwa wamejeruhiwa.

Watu wakishuhudia ajali hiyo, nje ya kituo cha treni

Watu wakishuhudia ajali hiyo, nje ya kituo cha treni

Waziri mkuu wa nchi hiyo Mostafa Madbouli ameapa kutoa adhabu kali kwa yeyote yule atakayehusika kupanga ajali hiyo.

Kwa upande wake, Rais wa nchi hiyo Abdul Fattah al Sisi ametuma salamu za rambirambi kwa familia za marehemu na kusisitiza kuwa watu wote waliojeruhiwa watapata msaada wowote watakaohitaji.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW