Burudani

Penny ameacha kazi E FM? Awaaga wasikilizaji wa Genge ‘kila jambo lina mwanzo na mwisho!’

Wasikilizaji wa kipindi cha ‘Genge’ cha 93.7 E-FM ya Dar es Salaam wamepokea kwa masikitiko taarifa kutoka kwa mtangazaji wa kipindi hicho waliyekuwa wamemzoea, Penniel Mungilwa a.k.a VJ Penny kuwa hatasikika tena kwenye kipindi hicho.

Penny1

Kupitia Instagram Penny ameandika:

“Gengerzzz hata sijui nianzie wapi, ila wacha niwaambie nawaona nyie wote kama familia yangu…toka day 1 mmekua na bonge la support! Message zenu ndio zilikua zinatuunganisha kama tunajuana…sina cha kuwalipa! I love u all beyond words!.. Sasa time yangu ya kufanya Genge imekwisha, ila sio ndio muondoke kimoja.. Mpeni support jamaa anaefuata, project zingine kali zinakuja ntawasanua, si mnajuanga napenda kuwapa vitu flani flani AMAZING??? I SALUTE ALL OF U…camp,unit, crew zote! Wadau wote mlitisha…kila jambo lina mwanzo na mwisho! Nimemaliza kazi yangu ya Genge..na wote mjipongeze kwa pamoja tulifanya vitu AMAZING…ALUTA CONTINUA! Baraka tele kwenu GENGERZ”

penny2
Penny akiwa mitamboni

Hizi ni baadhi ya comments za wasikilizaji ambao hawakuficha hisia zao baada ya kuagwa na mtangazaji aliyewaendeshea ‘Genge’ toka radio hiyo mpya ilivyoanza kuendesha vipindi mwaka huu.

-talaveencha: @vjpenny04 daaaah DAAAHHH hatuna CHA kusema kwako kubwa tunashukuru KWA sapot kubwa sana bila kubagua DAAH nahis kuchanganyikiwa ila tunasimamia pale pale RIZKI POPOTE NA WOTE TUPO CHINI YA JUA NA HAKUNA KINACHOSHINDIKANA NA KILA LIKUEPUKALO LINA KHERI NA WW INSHALLAH TUTAKUMISS

-teddykaegele: I’m sad my penny loved listening to u. @vjpenny04 mapenzi teleeee

-akidachodas: Uyu jamaaa cmuelewagi kiukweli bola niwe mkweli.abari zake myingi anazozisoma anazitoa #bongo5.sasa yeye kaz yake kuchukua abari uku ndo anatutangazia…

-nessaxa_david: Kwanini huo mda umekuwa mfupi sana ahhhh mi kwa upande wangu sijafurahia kutuonjesha vitu flaniflani amaizing afu ghafla hamna kitu ahhhh mj kazingua ahhhhh

-ney_ake: @vjpenny04 tumekuzoea mumytoo

-almasmzambele: Duh! Basi sawa ila roho inauma kimtindo @vjpenny04

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents