Michezo
Makundi ya timu 16 AFCON 2015 yatangazwa
Orodha ya makundi ya timu 16 zilizofuzu kucheza fainali za mashindano ya 30 ya kuwania kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015 imetoka. Mashindano hayo yatafanyika katika mji mkuu wa Equatorial Guinea, Malabo kuanzia Januari 17, 2015.
Awali michuano hiyo ilikuwa ifanyike nchini Morocco kabla ya kuhamishiwa nchini Equatorial Guinea. Mabingwa watetezi Nigeria ni moja ya timu kubwa zilizoshindwa kufuzu kucheza fainali za mwakani, pamoja na Misri na Angola ambazo zote kwa mshangao hazitaweza kushiriki.
Kundi A
Equatorial Guinea
Gabon
Burkina Faso
Congo Brazzaville.
Kundi B
Zambia
Tunisia
Cape Verde
Congo Drc
Kundi C
Ghana
Afrika Kusini
Senegal
Algeria
Kundi D
Ivory Coast
Cameroon
Guinea
Mali