Besta, Ray C, Lady Jay Dee na K-Lynn mna tatizo au!
Unapozungumzia wasanii wa kike hapa nchini, daima hawakamiliki kama hujawataja wasanii kama Besta, Lady Jay Dee, Ray C na K-Lynn ambao hawajawahi kusikika wamefanya kazi kwa ushirikiano kama ambavyo wanavyofanya wasanii wa mtoni au hata wasanii wa nchi jirani kama Kenya na Uganda.

Yaani haijawa kusikika kuwa msanii wa kike kumpa shavu msanii mwenzake wa kike kwani tatizo lenu nini? Hamuoni kama itapendeza sana iwapo mtaiga mfano kama wa wasanii wenzenu wa kiume ambao wamekuwa wakishirikiana mara kwa mara na kutengeneza mikono ya hatari? Na mfano hai ni mkono wa Mchizi wangu uliowashirikisha baadhi ya wasanii wakali katika miondoko ya Hip hop, huu ni mfano hai na unaostahiki kuigwa.
Acheni hizo dada zetu!?