Michezo

David Moyes ashtakiwa na FA kwa utovu wa nidhamu

Kocha wa klabu ya Sunderland ya Uingereza David Moyes ameshtakiwa na chama cha soka cha Uingereza kwa utovu wa nidhamu wakati wa mechi dhidi ya Southampton Jumatano.

39bf763000000578-3878140-david_moyes_was_sent_to_the_stands_against_southampton_after_swe-a-13_1477564361229

Southampton waliibuka na ushindi wa 1-0 katika kombe la EFL Cup uwanjani St Mary’s kupitia bao la Sofiane Boufal

Chama cha Soka cha Uingereza (FA) kimesema inadaiwa “Moyes alitumia lugha ya kutusi au maneno ya kuudhi akiyaelekeza kwa mwamuzi wa mechi.”

Kisa hicho kilitokea dakika ya 90 refa Chris Kavanagh alipokataa kuwapa Sunderland penalti baada ya mshambuliaji wa Sunderland Victor Anichebe kuonekana kuchezewa visivyo eneo la hatari.

Amepewa hadi saa tisa alasiri saa za Afrika Mashariki Jumanne kujibu tuhuma hizo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents