Burudani

Dully Sykes: Ukiimba wimbo wa kuelimisha Bongo imekula kwako

Hit maker wa ‘Inde’ na mtayarishaji wa muziki, Prince Dully Sykes amedai kuwa hapa Bongo kwa sasa ukiimba wimbo wa kuelimisha inakula kwako.

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa nyimbo zenye maneno ya tofauti na za kuchezeka ndio zinafanya vizuri tofauti na zile za kuelimisha.

“Tanzania ukitaka kuimba nyimbo za kuelimisha haitafanya vizuri. Mfano angalia kama Darassa wimbo wake unavyofanya vizuri kwa sasa. Watu wanaopenda muziki na wanaocheza ni watu wa usiku,” amesema Dully.

Muimbaji huyo ameongeza kuwa na yeye mwakani anakuja na lebo yake ambayo itakuwa inawasimamia wasanii na amewaahidi mashabiki wake kuja na wimbo mpya kuanzia mwezi wa kwanza mwishoni au wa pili mwanzoni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents