Michezo

Guardiola: Ubingwa wa EPL ni basi tena

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema kuwa timu yake kwa sasa inaweza kuondoka katika zile timu zinazowania ubingwa baada ya kupokea kipogo cha 4-0 kutoka kwa Everton.

Kwa sasa City wapo nyuma kwa alama 10 dhidi ya vinara Chelsea wenye alama 52.

Alipoulizwa kama alama 10 ni nyingi sana alijibu ndio sio rahisi kuzifikia.

Guardiola, ambaye ana miaka 45, amewaambia wachezaji wake kuungana wakati huu wa kipindi hiki kigumu na kutoangalia msimamo wa ligi mpaka mwisho wa msimu.

”Mwishoni mwa msimu tutajitathimini kiwango chetu,ufundishaji ulikuwaje na wachezaji walikuwaje.

Baada ya hapo tutaamua kwa pamoja.

Kocha huyo wa zamani wa timu za Barcelona na Bayern Munich amesema kuwa ana furaha sana kuwa ndani ya Manchester licha ya timu yake kuwa nafasi ya tano.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents