Michezo

Yanga hainitishi – Omog

Kocha wa klabu ya Simba SC raia wa Cameroon, Joseph Omog, ameweka bayana kwamba kamwe hatishiki na michezo yake iliyosalia kwa upande wa wapinzani wao Yanga na badala yake yeye anaangalia kikosi chake jinsi kitakavyoendelea kupata ushindi kwenye mechi zao.

Omog jana alikiongoza kikosi chake kupata ushindi dhidi ya African Lyon na kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara kikiwa kimebakiza mechi mbili.

Kocha huyo amesema kuwa kwake wala hana neno na hali hiyo kwani anaamini Yanga wanaweza kupoteza pointi kwa kuwa mechi hizo walizobakiza, baadhi ni dhidi ya timu ambazo zinapigana kutoshuka daraja, hivyo hazitataka kufungwa kirahisi.

Yanga imebakiza mechi dhidi ya Kagera Sugar, Mbeya City, Toto na Mbao.

“Kuwa mbele ya Yanga kimichezo kwangu wala hakuna kitu kinachoniathiri kwa sababu nimekita mawazo yangu katika kushinda mechi zetu na siyo kumuangalia mpinzani wetu anafanya nini au kabakisha idadi ya mechi ngapi.

“Kuwa na mechi nyingi kwa sasa sidhani kama ndiyo watatwaa ubingwa kwa sababu timu nyingi zinapigania kutoshuka daraja sasa unapokutana nazo zinacheza kufa na kupona kuhakikisha kwamba huzifungi na jambo hilo ndilo linalonipa imani kuwa wapinzani wetu hawatatufikia,” alisema Omog.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents