Habari
Lissu ameweza kula vizuri – Lema
Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema amesema kuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anaendelea vizuri na ameweza kula na kuongea na watu.
Mhe. Lema ametumia ukurasa wake wa Twitter kuelezea hali ya Mbunge huyo ambapo mara kwa mara amekuwa akitumia ukurasa huo kutoa taarifa za afya ya mbunge huyo.
“Mh Lissu anaendelea vyema hospital . Leo ameweza kula vizuri na kuongea na watu wengi zaidi. Asanteni kwa sala zenu. Mungu awabariki sana,” ametweet Lema.
Mbunge Lissu aliyejeruhiwa tarehe 7, Septemba kwa kupigwa risasi eneo la ‘area D’ mjini Dodoma na watu wasiojulikana.