Michezo

Azam FC vs Kagera Sugar kibaruani leo

Duru la tatu la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, linatarajiwa kuendelea mwishoni mwa wiki hii ambapo kwa mujibu wa ratiba ya ‘VPL’, leo siku ya Ijumaa Azam FC itaialika Kagera Sugar majira ya saa 1.00 usiku (19h00) katika Uwanja wa Azam Complex Jijini Dar es salaam.

Siku ya Jumamosi Septemba 16, 2017 Majimaji FC ya Songea itacheza na Young Africans ya Dar es Salaam, saa 10.00 jioni (16h00) katika Uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.

Mbao itasafiri hadi Manungu mkoani Morogoro kucheza na Mtibwa Sugar katika mchezo ambao pia utapigwa Jumamosi saa 16h00 wakati Tanzania Prisons ya Mbeya itakuwa mwenyeji wa Ndanda FC saa 16h00 kwenye Uwanja wa Sokoine.

Lipuli Fc itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting saa 16h00 katika Uwanja wa Samora, Iringa wakati Stand United itacheza na Singida United saa 16h00 kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Siku ya Jumapili Septemba 17, 2017 Mbeya City itaikaribisha Njombe Mji saa 16h00 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya huku Simba SC ikiwa mwenyeji wa Mwadui FC saa 16h00 jioni katika Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents