Michezo

Thabani Kamusoko yupofiti – Dr Edward

Daktari wa wachezaji wa klabu ya Young Africans, Dr Edward Bavu amethibitisha kuwa kiungo wa timu ya taifa ya Zimbabwe, Thabani Michael Kamusoko yupo tayari kwa mikiki mikiki ya Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kupatiwa matibu na hivyo ni jukumu la benchi la ufundi kuamua kumchezesha katika mchezo utakao pigwa leo dhidi ya Majimaji FC Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Dr Edward Bavu ameuambia mtandao wa klabu ya Dar es salaam Young Africans kuwa “Sina shaka nae tena jioni amefanya mazoezi vizuri ni jukumu la benchi la ufundi kuamua kama anaweza kuwa sehemu ya kikosi kitakachoanza”.

Katika duru la kwanza la Ligi kuu Tanzania bara Yanga SC ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Lipuli FC mchezo uliyochezwa katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam Agosti 27 mabao yaliyofungwa na Seif Abdallah upande wa Lipuli huku kwa Yanga likiwekwa kimyani na Donald Ngoma.

Wakati mchezo wa duru la pili klabu ya Yanga ilichomoza na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Njombe Mji bao lililofungwa na mchezaji mpya wa timu hiyo akitokea Simba SC, Ibrahim Ajib.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents