HabariUncategorized

LHRC wamuomba Rais Magufuli kufuta adhabu ya kifo (+Video)

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) wanaungana na mtandao wa kupinga adhabu ya kifo duniani katika maadhimisho ya 15 ya siku ya kupinga adhabu ya kifo duniani huku wakimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kwa kuweka wazi msimamo wake wa kutokuunga mkono adhabu ya kifo hasa kwa imani yake binafsi.

Kaimu Mkurugenzi wa Utetezi wa Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), Bi. Anna Kenga

Akizungumza na waandishi wa habari, leo jijini Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Utetezi wa kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), Bi. Anna Kenga  amesema kuwa adabu hiyo ni ya kikatili ambayo inakinzana na misingi ya utu na misingi ya haki za binadamu kama ilivyoainishwa katika matamko na mikataba mbalimbali ya Kimaifa.

Hata hivyo Kituo hicho kimetoa mapendekezo yafuatayo;

1- Serikali itekeleze pendekezo la mpango wa kujitathmini wa nchi wanachama wa umoja wa Mataifa(universal periodic review) mwaka 2016 kwa kuridhia mkataba wa nyongeza wa haki za kiraia na kisiasa na kutangaza rasmi sasa kuwa haitekelezi adhabu ya kifo.

2-Serikali irekebishe sheria ya kanuni na sheria ya adhabu ya ugaidi yenye kutoa adhabu ya kifo kwa makosa ya mauaji, uhaini na ugaidi.

3-Serikali kutokutunga au kubdilisha sheria nyingine na kuongeza adhabu ya kifo kama ilivyofanywa kwenye sheria ya ugaidi ya mwaka 2002 kwa mwaka huu

4-Serikali itengeneze taratibu ya kuelimisha jamii juu ya kuheshi haki za binadamu hususani haki za kuishi na kuweka mazingira ya uheshimuji wa haki hiyo.

5-Serikali ibadilishe sheria na kuondoa adhabu ya kifo na kuweka adhabu mbadala kwenye makosa ya jinai

6-Kwa vile utekelzaji wa sheria hii una mkera Rais basi awe kinara katika kuitisha mabadiliko haya ili yeye na Majaji waondolewe mzigo wakutekeleza adhabu hii mbaya na kutweza utu wa mtu.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents