Habari

Mwanafunzi kidato cha 3 akamatwa na sare za JWTZ(+video)

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, linamshikilia  Said Selemani (17)  mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Fahari iliyopo Goba kwa kosa la kukutwa na sare za JWTZ (Kombat).

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum hiyo, Lazaro Mambosasa amesema kuwa mwanafunzi huyo alikamatwa huko maeneo ya Mbezi CRDB bank akiwa amevaa sare hizo za JWTZ huku akivuta sigara hadharani na kufanya vitendo vingine ambavyo haviendani na maadili ya askari aliyevaa sare.

Aidha Kamanda Mambosasa amesema katika mahojiano ya awali kijana huyo alijitambulisha ni askari toka kikosi cha 501 KJ kilichopo Lugalo jijini Dsm,baada ya kubanwa zaidi alikiri kupata uniform hizo toka kwa rafiki zake anaokuwa nao sehemu mbalimbali.

Hata hivyo kijana huyo  alipopekuliwa katika begi la mgongoni alilokuwa nalo alikutwa na kofia nyingine moja pamoja na kitambulisho namba DFF 7001A cha familia ya askari chenye namba 1231 ambacho ni cha mtoto wa askari wa JWTZ MT 65640 Private GABRIEL KIHWILI wa 501 KJ kikiwa na picha ya mtoto wake ELIA GABRIEL.

Kamanda Mambosasa amesema kuwa uchunguzi bado unaendelea ili kuwapata rafiki zake hao ambao inadhaniwa kuwa huwa wanashirikiana katika kufanya matukio ya kihalifu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents