Mitindo

Fahamu kuhusu begi mpya mjini ziitwazo Fanny Pack

Je unaijua Fanny Pack bagi mpya mjini inayofanya poa kwa sasa katika ulimwengu huu wa mitindo? Leo Bongo 5 uitakupatia dondo chache kuhusu begi hiyo ambyo utumiwa na wakaka pamoja na wadada.

Aina hii ya bag zipo mida mrefu sema kuboreshwa kwake ndio kunafanya leo niukupe dondo nzuri kabisa ziatakazoweza kukupa muongozo wa kumiliki pamoja na kuzitumia. Awali wengi walizitumia begi hizi kama za mazoezi kwa kuweka pesa kiduchu ama kitambaa kwa ajili ya kujifuta jasho wawapo mazoezini.


Lakini leo naweza kuthubutu kusema kuwa bag hizi ni moja ya begi zinzaofanya poa kwa sasa katika ulimengu wa mitindo kwani zimeboreshwa na kuwa nzuri zaidi ambapo zinakupa hamsa ya kutaka ku-roll nazo katika mitoko yako.


Aina hii yap begi uvaliwa tumboni na mikata yake ufunga kwa nyuma ili isiweze kudondoka, Ila wengine uvaa Funny Pack katika kiuno na vile vile utumia kama mkanda wa nguo.

Ukiwa unayo begi hii na unahitaji kutoka nayo hakikisha kuwa umeweka vitu vicheche na vyenye umuhimu kama vile, ATM Cards, Vitambulisho vyako, pesa kidogo, simu ya mkononi, chaji, kitambaa cha jasho na simple makeup kit kwa wadada.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents