Muingereza, Brewster azua gumzo kwa kukosea neno ‘unstoppable’ kwenye tattoo yake (+Picha)
Muingereza, Brewster azua gumzo kwa kukosea neno 'unstoppable' kwenye tattoo yake (+Picha)
Mchezaji wa klabu ya Liverpool raia wa Uingereza, Rhian Brewster amezua gumzo kwenye vyombo mbalimbali vya habari baada ya kuonekana kukosea neno ‘unstoppable’ kwenye ‘tattoo’ yake aliyochora kwenye mkono.
Mapema hii leo, Brewster mwenye umri wa miaka 18 ametupia picha inayomuonyesha akiwa kwenye uzi wa Liverpool huku mkono wake wa kushoto kukiwa na ‘tattoo’ hiyo yenye maneno yanayo someka ‘your hate makes me unstoppable’ (Chuki zako haziwezi kunizuia).
Kwenye tattoo hiyo iliyopo chini ya mchoro wa mpira na dunia imekosewa herufi moja imeandikwa ‘unstopable’ ikipungua herufi ‘p’ moja badala ya neno sahihi ‘unstoppable’.
Wachambuzi wa mambo wanadai kuwa tattoo hiyo ni mpya kwenyemwili wa Brewster kutokana kutokuonekana nayo wakati wa mchezo wa fainali ya michuayo ya kombe la dunia kwa vijana waliyo na umri chini ya miaka 17 wakati timu ya taifa ya Uingereza ilipotwaa taji hilo nchini India mwezi Oktoba mwaka jana.