Mitindo

Odemba aja kishujaa

MSHINDI wa pili wa mashindano ya Miss Earth, Miriam Odemba jana alipokelewa kwa vishindo aliporejea kutoka nchini Philipines alipokwenda kushiriki mashindano hayo

Miriam Odemba akionesha Crown yake original kabisa aliovishwa mara baada ya kuibuka mshindi wa pili katika mashindano ya Miss Earth Air 2008 yaliyofanyika nchini Filpine hivi karibuni

MSHINDI wa pili wa mashindano ya Miss Earth, Miriam Odemba jana alipokelewa kwa vishindo aliporejea kutoka nchini Philipines alipokwenda kushiriki mashindano hayo.

Odemba aliwasaili jana mchana, alipokelewa kwa kwa matarumbeta huku Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere ukiwa na shangwe kupindukia.

Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Alex Masinde na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Peter Mwenguo waliongoza wadau wa urembo kumpokea Odemba ambaye ameiwakilisha vyema Tanzania katika mashindano hayo.

Wengine waliokuwepo ni wadau wa urembo, ndugu na jamaa zake pamoja na mama yake mzazi, Margareth Odemba.

Akizungumza na waandishi wa habari, Odemba alianza kwa kuishukuru kampuni ya Compass Communications kwa kumpa nafasi na kumwandaa vyema kwa ajili ya mashindano hayo na kushika nafasi ya pili.

 

Source: Mwananchi

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents