Habari

Video: Nyumba 32 za bomolewa Dar, wananchi walala nje, wadai waliingizwa mkenge na kiongozi wa Mtaa

Wananchi wa Kitongoji cha Yangeyange Kata ya Msongola Ilala jijini Dar es salaam wamejikuta wakiwa katika wakati mgumu baada ya nyumba zao zaidi ya 32 kubomolewa na kampuni moja ya udalali iitwayo, Lumina kwa madai kwamba wamepewa oda hiyo na Mahakama baada ya mteja wao ambaye anajulikana na kwa jina moja, Scolastica kushinda kesi ya uvamizi katika viwanja hicho.

Tukio hilo limetokea tarehe 9 Machi 2019 na mpaka sasa Wananchi hao pamoja na watoto wao wanalala nje chini ya miti katika eneo.

Wananchi hao wanadai kwamba hawakuwa na taarifa ya kwamba viwanja nyao vipo kwenye migogoro na kesi ipo Makahamani mpaka walivyokuja watu hao na kuanza kubomoa.

Akiongea na mwandishi wetu, mmoja kati ya wahanga wa tukio hilo aitwaye, Pendo Masanja alidai yeye alinunua eneo hilo toka mwaka 2016 chini ya viongozi wa serikali ya Mtaa na alianza kujenga tararibu mpaka alivyomaliza na kuhamia na familia yake.

“Sikuwahi kusikia kwamba eneo hili lina mgogoro toka nimekuja hapa, nimeanza kujenga mpaka nimemaliza na nimetumia zaidi ya tsh milioni 50. Leo hii imeenda kazini imeacha watoto nyumbani narudi mchana nakuta nyumba imebomolewa imeumia sana, kila kitu kimepotea, naomba tusaidiwe tuna watoto,” alisema Pendo.

Naye kikongwe mwenye miaka 72 Violet Philipo Chumburu ambaye ni mjane, pia ni mstaafu wa BOT, amedai kwamba yeye baada ya kustaafu kazi alinunua eneo hilo kutoka kwa raia wa eneo hilo na kuandikilishiana mpaka kwa viongozi wa serikali za mtaa.

“Nitaenda wapi jamani mimi mstaafu sina pesa tena nilijenga nyumba yangu nikasema hapa nitakaa mpaka Mungu atakaponichukua, sina jinsi tena naomba serikali, Paul Makonda pamoja na Rais Magufuli ambaye nilimpigia kura aingilie kati suala hili hatuelewi hawa watu wametoka wapi,”

Baada ya sakata hilo Bongo5 ilimtafuta Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo aitwae, George Muhele ambapo yeye alidai kwamba hakuwa na taarifa yoyote kwamba nyumba za eneo hilo zinaenda kuvunjwa.

“Kwanza sikuwa na taarifa kwamba kuna bomoabomoa katika mtaa wangu mpaka nilivyopigiwa simu na Wananchi wangu na kwenda eneo la tukio nikakuta kuna nyumba 16 tayari zimeshabomolewa. Baada ya kufika kuwauliza wakawa wakali sana, wakanionyesha barua ya mkuu wa polisi, lakini barua nyingine ya kuruhusiwa kubomoa sikuipata mpaka leo kwa sababu Mahakama ikitoa oda ya kubomoa toka mwaka 2018, lakini ile oda haitekelezwi mpaka ipite kwa DC na viongozi wengine na baadae wakija kwenye eneo husika lazima nionyeshwe na mimi niwaambie wananchi wangu, lakini hawakufanya hivyo,”

Kuhusu uhalali wa eneo hilo, Mwenyekiti huyo alisema “Hawa wananchi hawana hatia, wao walinunua viwanja kutoka kwa wavamizi ambao walipora shamba hilo kutoka kwa mwenyewe mwaka 2015 na hawa watu walivyokuwa wanaenda kununua eneo hawapiti huku, nasikia tu kuna baadhi ya wajumbe wangu wanahusishwa mimi sipo na hao tukiweza kuwabana vizuri wataeleza mihuri ya ofisi yangu waliipata wapi kwa sababu siku hizi kuna watu wanafoji vitu, juzi tumemkamata mtu akiwa na muhuri wa serikali ya mtaa na hatujui aliupata wapi,”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents