Burudani

Msimu mpya wa BSS wazinduliwa rasmi: Idris Sultan mtangazaji, Dully Sykes na Lady JayDee majaji wapya (+Video)

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Benchmark Productions na Jaji Mkuu wa shindano la Bongo Star Search, Rita Paulsen leo Septemba 17, 2019 ametangaza kuzindua rasmi msimu mpya wa 10 wa shindano hilo.

Akiongea na Waandishi wa Habari, Madam Rita amesema kuwa shindano la mwaka huu, Litakuwa na majaji wapya wawili, Ambao ni Dully Sykes na Lady Jaydee watakaoshirikiana na Jaji Mkuu Madam Rita na Master Jay.

Kwa upande wa mtangazaji wa msimu mpya wa BSS, Madam Rita amesema kuwa mchekeshaji Idris Sultan ndiye atakayekuwa mtangazaji msimu huu wa 10.

Akitaja mchakato wa usaili, Rita Poulsen amesema ujio wa msimu wa kumi huku akitaja ongezeko la mikoa ambayo itafikiwa na usaili wa shindano hilo.

“Nina furaha sana kwa sababu ni ‘anniversary’ ya miaka 10 ya Bongo Star Search, najivunia vipaji ambavyo tumevileta mbele ya watanzania na kuwapa nafasi vijana hao wa kitanzania kuendeleza maisha ya kimuziki na wengine kufanikiwa nje ya muziki pia”. amesema Rita Poulsen, Jaji Mkuu BSS na Mkurugenzi Mkuu wa Benchmark Productions.

“Habari njema sana kwa watanzania ni kwamba tumeongeza idadi ya mikoa ambayo itafikiwa na usaili wa BSS mwaka huu, Mwaka huu tunakwenda Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma na Dar es Salaam. Jumla mikoa mitano tofauti na mwaka jana tulipokwenda kwenye mikoa mine pekee”. Amesema Madam Rita.

Usaili wa kwanza utafanyika jijini Arusha tarehe 28 – 29 mwezi Septemba, Mwanza tarehe 4- 5 Oktoba, Mbeya tarehe 10 – 11 Oktoba, Dodoma tarehe 17 – 18 Oktoba na Dar es Salaam tarehe 23, 24, 25 Oktoba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents