Burudani

”Nandy yupo katika tamthilia ya Huba, Wolper ndani ya Sarafu, Dully Sykes ataigiza” – Hilda Nakajumo wa DStv

Baada ya kuwashangaza wateja wake kwa punguzo kubwa la bei ya vifurushi vya DStv, Kampuni ya MultiChoice Tanzania imefungua mwaka kwa ofa ya aina yake, ambapo sasa mteja akilipa kifurushi chake huzawadiwa kifurushi cha juu yake bila malipo ya ziada. Mkuu wa tengo cha thamani kwa wateja Hilda Nakajumo akizungumza na Bongo5 amesema sasa watu wataweza kumuona Nandy katika tamthilia ya Huba, Jacqueline Wolper akiwa kwenye Sarafu basi huwenda msanii Dully Sykes akaonekana kwenye maigizo badala ya muziki pekee.

Ofa hii ambayo imepewa jina la Kitu juu ya Kitu imeanza rasmi ambapo sasa mteja wa DStv akilipa kifurushi chake cha juu yake bila gharama zaidi na hivyo kuweza kupata chaneli za kifurushi cha juu kuliko kile alicholipa.

Hilda Nakajumo amesema ofa hiyo ni kwa wateja wote wa DStv kuanzia kifurushi cha Bomba hadi wale wa kifurushi cha Compact Plus. ”Ofa hii ni mahsusi kwa wateja wetu wa kuanzia kifurushi cha Bomba hadi Compact plus na kila mteja atakayelipia kifurushi chake atapandishwa daraja kwenda kifurushi cha juu yake ndani ya muda wa saa 48.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents