Michezo

RC Makonda: Mh Rais kijana wako Samatta amesajili kwenye timu kubwa, matokeo ya jana Yanga 3-1 Singida yameongeza amani (+Video)

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mh Paul Makonda amemwambia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli juu ya usajili mkubwa wa Mshambuliaji na Nahodha wa Tanzania na mchezaji wa klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta kutua ndani ya timu ya Aston Villa inayoshirki ligi kuu England. Makonda ameyasema hayo wakati wa Hafla ya kukabidhiwa nyumba za maafisa na askari wa Magereza Ukonga jijini Dar Es Salaam.

RC Makonda: Mh Rais kijana wako Samatta amesajili kwenye timu kubwa, matokeo ya jana Yanga 3 – 1 Singida yameongeza amani (+Video)

”Lamwisho Mh Rais ni swala zima la amani katika Mkoa wetu. Naomba nikuhakikishie Mh Rais Mkoa unaenda vizuri, umetulia, unaamani ya kutosha. Naamani inazidi kuongezeka baada ya matokeo ya jana ya Yanga kupata 3 – 1 kule Singida.”- Amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Makonda.

Paul Makonda ameongeza ”Kwahiyo Mh Rais ufahamu tu ya kwamba, mambo haya pia yanaongeza utulivu katika Mkoa wetu. Lakini zaidi ya yote kijana wako amesajili kwenye timu kubwa, ambaye ni Nahodha kwenye timu yetu ya taifa, Mbwana Samatta sasa hivi anapeperusha bendera ya Tanzania katika dunia nyingine. Na kwa kweli ni heshima kwa Taifa letu, heshima kwa Samatta mwenyewe na familia yake, lakini kubwa kuliko ni heshima kwako Mh Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli.”

”Ni matumaini yetu huko mbele ya safari, iko siku timu hiyo itatuwa katika dimba la Mkapa kuchuana na timu yetu moja bingwa alafu tunawachukua tunawapeleka kwenye mbuga za wanyama wakajionee ufahari na utajiri wa Taifa letu, ili wanapocheza kwenye ligi kuu huko kwenye ligi yao waweze pia kutangaza Tanzania.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents