Habari

Remdesivir yaidhinishwa kutibu virusi vya Corona Ulaya

Tume ya Ulaya hii leo imeidhinisha matumizi ya dawa ya kupambana na virusi inayoitwa remdesivir, kutibu virusi vya corona kwa mujibu wa Kamishna wa Afya wa Umoja wa Ulaya Stella Kyriakides.

Ägypten Kairo | Coronavirus | Medikament Remdesivir (Reuters/A. Abdallah Dalsh)

Kyriakides amesema katika taarifa yake, kwamba idhini hiyo iliyotolewa leo ni hatua muhimu katika mapambano na virusi hivyo.

Tafiti mbili za Kimarekani zimeonyesha kuwa dawa ya remdesivir, inaweza kupunguza muda wa kukaa hospitalini kwa wagonjwa wa COVID-19. Kwa wastani, inapunguza wagonjwa kubakia hospitalini kutoka siku 15 hadi 11.

Mnamo Mei mosi, Marekani iliruhusu matumizi ya dharura ya dawa hiyo, ambayo hapo awali ilikusudiwa kutibu ugonjwa wa Ebola. Na baadae zilifuatia nchi za Asia, ikiwa ni pamoja na Japan na Korea Kusini.

Source, Deutsche Welle

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents