Promotion
Jisajili na ZAIN ushinde zawadi
Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi, ZAIN, leo imezindua promosheni itakayowazawadia wateja wake watakaosajili namba zao kabla ya zoezi hilo kufikia mwisho Oktoba 15 mwaka huu, dakika 30 za bure za muda wa maongezi.
Meneja huduma wa kampuni ya simu ya mkononi ya zain Bw. Gabriel Kamukura alikizungunza na wandishi wa habari leo makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam alisema kuanzia leo mteja wa Zain atakayesajili laini yake atapatiwa muda wa wa dakika 30 ambazo atazitumia ndani ya siku mbili ikiwa ni moja ya changamoto zinazotolewa na kampuni hiyo.
Bw. Gabriel amesema mpaka sasa hivi ni asilimia 75 ya wateja wa zain tayari wameshajisajili na asilimia 25 ndiyo iliyobaki, Zain ina wateja milioni 7.500.000 nchini.