Habari

Jarida la Forbes limetoa orodha ya watu 100 maarufu wenye nguvu zaidi duniani 2013. Oprah, Lady Gaga, Beyonce, Rihanna washika nafasi za juu

Jarida la Forbes jana (June 26) limetoa list ya watu 100 maarufu wenye nguvu zaidi duniani 2013, na maceleb wa kike wamejibu swali la wimbo wa Beyonce Knowles “Who run the world”, of course kwa mujibu wa orodha hii ya Forbes jibu ni “Girls”.

celebs

Oprah Winfrey, Beyonce Knowles, Lady Gaga & Rihanna ni miongoni mwa maceleb wa kike waliofanikiwa kukamata nafasi za juu katika list hiyo ya ‘100 MOST POWERFUL CELEBRITIES IN THE WORLD 2013’.

Vigezo ambavyo Forbes wametumia safari hii kuwapata ‘most powerful celebrities’ sio vipato vyao vya kifedha moja kwa moja, bali wametumia ‘umaarufu’ wa star husika.

Kwa Forbes ‘umaarufu’ wameutafsiri kama nguvu inayopimwa na kipato cha star kwa miezi 12, kwa kiasi gani star ametajwa katika vyombo vya habari magazeti na TV, na uwepo au ushiriki wa star katika mtandao.

Kwa vigezo hivyo vya Forbes, media mogul Oprah Winfrey ndiye amekamata nafasi ya kwanza katika list hiyo akiwa ndiye mtu maarufu mwenye nguvu zaidi duniani 2013(kwa mujibu wa forbes), akifuatiwa na Lady gaga ambaye amekamata nafasi ya 2, wakati mke wa Jay Z Beyonce amekamata nafasi ya 4 akifuatiwa na Madonna katika nafasi ya 5.

Wengine ni Taylor Swift katika nafasi ya 6, Justin Bieber katika nafasi ya 9, Jennifer Lopez katika nafasi ya 12 na nafasi ya 13 imekamatwa na Rihanna.

Itazame list nzima ya top 20
forbes100

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents