Lil Wayne aiua soo ya kuikanyaga bendera ya Marekani kwenye video ya God Bless Amerika
Video mpya ya wimbo wa boss wa Young Money Lil Wayne unaoitwa “God Bless Amerika” imetoka jana. Wakati wa utengenezwaji wa video hiyo kuna skendo iliibuka baada ya Weezy kuonekana akiikanyaga kanyaga bendera ya Marekani kama tambala bovu, tukio ambalo lilikamatwa na kamera japo baadae alijitetea mara hakuiona ikiwa chini, mara halikuwa lengo lake japo script ya video ilitaka bendera ionekane inadondoka kwa nyuma yake na sio kuikanyaga.
Lil Wayne “God Bless Amerika” from EIF RIVERA on Vimeo.
Well it’s all good, kuna uwezekano timu yake imemshauri na wakafanya uamuzi wa busara kwa kutovitumia kabisa vipande vinavyoonesha akidhihaki bendera ya taifa lake kwa kuikanyaga kanyaga, so the dude is clean!
Tazama hapa Video ya wakati Lil Wayne alipoikanyaga bendera hiyo wakati wa utengenezwaji wa video hiyo
http://youtu.be/B8P6ZuUwX5k