Habari

Mtoto wa Usher alazwa ICU baada ya kupata ajali kwenye bwawa la kuogelea

Mtoto wa kiume wa Usher, Usher Raymond V mwenye umri wa miaka mitano amelazwa hospitali baada ya kupata ajali kwenye bwawa la kuongea jana.

article-2385570-1B2D17E1000005DC-510_634x843

Vyanzo vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa ajali hiyo ilitokea mida ya saa 12 jioni. Mtoto huyo alipelekwa moja kwa moja ICU kwenye hospitali ya jijini Atlanta. Usher hakuwepo nyumbani wakati wa tukio hilo.

usher-sons-bw

Kutokana na ajali hiyo imedaiwa kuwa mapafu yake yalijaa maji. Usher Raymond V, ambaye Usher humwita Cinco, ni mtoto wa kwanza aliyezaa na mke wa zamani Tameka Raymond. Wazazi hao wote wapo hospitali kufuatilia afya ya mtoto wao.

Mwaka jana mtoto wa mke wake huyo wa zamani, Kile alifariki kutokana na kugongwa na boti.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents