Abdul anyakua mil.10!!

Abdul anyakua mil.10!!
Abdul Hafidh aka "Rick Ross", ambaye alikuwa miongoni mwa washiriki
kumi wa shindano la Maisha Plus, lililokuwa likionyeshwa moja kwa moja
na kituo cha televisheni cha TBC1, juzi usiku aliibuka mshindi.

Kutokana na ushindi huo, Abdul ambaye
alikuwa mshiriki pekee kutoka Zanzibar, huku tisa wakitoka Tanzania
Bara, amejinyakulia kitita cha sh mil 10 zilizotolewa na mmoja wa
wadhamini wa shindano hilo, Infinity Communications ya jijini Dar es
Salaam.

Abdul, wakati wote wa shindano hilo aliweza kuvuta hisia za mashabiki
wengi kutokana na kujituma kwenye kazi pamoja na ucheshi wakati
alipokuwa kijijini na wenzake, hivyo kufanya ushindi wake kupokelewa
bila manung’uniko.

Mbali ya Abdul, washiriki wengine ambao walikuwa kivutio, ni Upendo
Peneza wa Mwanza, ambaye aliweza kuingia katika tatu bora za shindano
hilo ambapo washiriki walikuwa wakipigiwa kura na mashabiki.

Nafasi ya pili ilinyakuliwa na Ngaja, ambaye alipopewa nafasi ya kutoa shukrani, alisema kuwa Abdul alistahili kushinda.

Naye Upendo alisema kuwa roho yake imeumia kwa kuzikosa sh mil.10,
lakini anashukuru kwamba amejifunza mengi katika kijiji hicho.

Wengine walioingia kumi bora katika shindano hilo lililoanza Machi
Mosi, ni Boniface Michael, Hamis Mohammed ‘Kingunge’, Modesta Peter,
Moshy Mahona, Steve Sandhu na Teddy Mhando.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents