Burudani

Afya ya DMX yazidi kutetereka

Hali ya rapper wa Marekani, DMX inazidi kua mbaya – amevunja ziara ya show zake za wiki hii.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, tayari rapper huyo mkongwe amevunja show zake alizotakiwa kufanya Jumatano mjini Los Angeles na ya San Diego aliyotakiwa kuifanya Alhamisi ya leo. Show ya kwanza kuvunjwa ilikuwa ya Santa Anna, California aliyotakiwa kuifanya siku ya Jumanne.

Afya ya DMX ilionekana kua mbaya kuanzia wikiendi iliyopita akiwa na kundi lake la Ruff Ryders.Wakati wa show hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Barclays Center, Brooklyn, rapper huyo hakufanya kile kilichotarajiwa na mashabiki kutokana na afya yake kutetereka akiwa stejini.

Inadaiwa kuwa, kuzorota kwa afya ya DMX inatokana na matumizi ya pombe kali na dawa za kulevya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents