MichezoUncategorized

Aden Rage akana kkuwania nafasi ya Urais wa TFF

Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Alhaji Ismail Aden Rage amekanusha nia ya kugombea cheo chochote ndani ya shirikisho lenye dhamana ya kusimamia mchezo wa soka nchini TFF.

Rage amesema kwamba yaliyosemwa ni maneno ya uzushi, na anatarajia tu kuwa mwanachama muaminifu ndani ya klabu yake ya Simba SC.

Mwenyekiti huyo anayeaminika kuifahamu sheria, amekiri pia Matajiri wa soka Mkoa wa Dar es salaam, wakoka mikate, klabu ya soka ya Azam, si ya kubezwa kwani ni klabu nzuri na yenye uwezo wa kuwashangaza watu katika mchezo wa shirikisho utakaochezwa siku ya jumamosi na hivyo kuwasihi vijana wake Msimbazi kuuwekea umakini mchezo huo.

Aden Rage ambae alishawahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya soka ya Simba, na kuwa Mbunge wa Tabora Mjini, amewahasa wanachama na wapenzi wa Simba SC kujitokeza uwanjani kuishangilia klabu yao kwa kuwa ni mchezo mzuri hasa zinapokutana timu hizi mbili. Simba itajitupa uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa michezo miwili ndani ya mwaka mmoja na klabu hii ya Azam, ambapo mchezo wa kwanza visiwani Zanzibar na wa pili ni katika ligi kuu Soka Tanzania Bara.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents