Habari

Afya ya shahidi yakwamisha kesi ya Sabaya

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imelazimika kuahirisa kesi ya Uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita kutokana na shahidi kuendelea kusumbuliwa na tumbo.

Wakili Mwandamizi wa Serikali, Felix Kwetukia ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha iahirishe kesi hadi Oktoba 27, 2021 kwa kuwa shahidi huyo afya yake bado haijaimarika.

Shahidi huyo ambaye ni Afisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Ramadhan Juma alitegemea kutoa ushahidi wake tangu jana Alhamisi  Oktoba 21, pia leo 22, 2021, lakini imeshindikana kutokana na maradhi hayo ya tumbo.

“Mahakama imeona uthibitisho wa kuugua kwa shahidi wa saba umeletwa na muda wa kutoa hati ya wito kwa mashahidi wengine umekuwa mfupi, hivyo mahakama imeona busara kuahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 27, 2021” Hakimu Mkazi, Patricia Kisinda.

Awali Mawakili wa utetezi walipinga ombi hilo na kuiomba mahakama iamuru Jamhuri iwalete mashahidi wengine ili shauri hilo liendelee kusikilizwa.

BY : Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents