Michezo

Aguero aandika ujumbe mzito baada ya kunusurika kifo

Mshambuliaji wa timu ya taifa Argentina na klabu ya Manchester City, Sergio Leonel “Kun” Aguero ameandika ujumbe mzito wa shukrani baada ya kunusurika kifo kupitia ajali ya gari aliyopata  juzi siku ya Alhamisi katika  Jiji la Amsterdam huko nchini Uholanzi.

Kun Aguero, ambaye amepata ajali hiyo masaa machache baada ya kuudhuria tamasha la mwanamuziki raia wa Colombia, Juan Luis Londono Arias maarufu kama ‘Maluma’ lililofanyika Amsterdam, ameandika ujumbe huo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter na Instagram akiwashukuru wote waliyomhudumia wakati wote na waliyotumia muda wao kumtakia ahuweni.

“Kwa sasa nipo nyumbani kwangu Jijini Manchester baada ya kufanyiwa vipimo na madaktari wa klabu nimevunjika mbavu licha ya maumivu niliyonayo lakini naendelea vizuri na mawazo yangu yote nimeyaweka katika kupata kupona haraka ahsanteni wote.”Amesema Aguero nyota wa Man City.

Kun Aguero ameongeza “Ahsanteni sana kwa barua nyingi mlizonitumia zikiwa zinanitakia ahuweni na kupata kupona haraka lakini pia napenda kushukuru kwa huduma nzuri niliyoipata VU University Medical Amsterdam.”

Aguero apata ajali mbaya ya gari Uholanzi

Mshambuliaji huyo amefunga jumla ya mabao saba katika michezo nane aliyocheza msimu huu na kumsaidia kocha wake, Pep Guardiola kuwa katika nafasi nzuri ya msimamo wa Ligi ya Uingereza na kushinda michezo ya Klabu bingwa barani Ulaya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents