Burudani

Aina ya msanii anayemtaka Laizer wa WCB studio

Producer kutoka label ya WCB, Laizer ametaja sifa za msanii ambaye anapendelea kufanya naye kazi studio.

Laizer ambaye ametoa hit songs kibao za wasanii wa WCB amekiambia kipindi cha Clouds E kuwa anapenda kufanya kazi na msanii ambaye anapenda kuchangia chochote katika kile ambacho kinafanyika na si kumuachia producer pekee yake.

“Napenda msanii ambaye yupo haraka kufanya kitu, anaweza akaja na idea yake, hata kama nitafanya mwenyewe lakini pia akawa ni mtu ambaye anaweza kuchangia mawazo katika kazi yake siyo kwamba amekuachia producer umalize kila kitu, napenda msanii wa namna hiyo” amesema Laizer.

Katika hatua nyingine amezunguzia safari yake katika tasnia ya muziki hadi kuwa producer kwa kusema mwanzo alikuwa msanii ndipo baadae kujeukia upande wa pili.

“Nilikuwa naona kuna usumbufu fulani hivi nilikuwa naupata nikienda kwa producer ratiba zile haziko sawa, kwa hiyo nikatamani kama nikijifunza nitakuwa najitengenezea mwenyewe” amesema Laizer.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents