Habari

Ajali ya basi yaua watu 12 Tabora

Watu 12 wamefariki dunia na wengine 46 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la abiria la City Boy kugongana uso kwa uso na fuso usiku wa kuamkia leo, Aprili 05, 2018 Igunga mkoani Tabora, ambapo Basi la City Boy lilikuwa likifanya safari yake kutoka Karagwe kwenda Dar es Salaam.

3.jpg

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Wilbrod Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na tayari majeruhi wamepelekwa hospitali.

Jumla ya watu 12 wamepoteza maisha , 10 eneo la tukio, 2 wakiwa wanapelekwa Hospitali ya Wilaya Igunga. Jumla ya majeruhi 46 wamefikishwa Hospitali ya Wilaya Igunga kwa matibabu, kati yao 3 ni mahututi ambapo ME 02 wamepelekwa Bugando Mwanza na KE 01 amepelekwa Nkinga usiku huu.“amesema Kamanda Mutafungwa.

Hata hivyo, jeshi la polisi limeahidi kutoa taarifa zaidi leo baadaye ikiwemo na hali ya majeruhi wa ajali hiyo.

Kufuatia ajali hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambi rambi kwa familia zilizopoteza ndugu, jamaa na marafiki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents