Habari

Suala la wakina baba kubambikiziwa watoto lazua gumzo bungeni (+video)

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa si kweli kwamba watoto sita kati ya watoto waliopo nao wakina baba sio wa baba huyo au wazazi husika.

Dkt. Ndugulile ametoa kauli hiyo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge Busega, Raphael Chegeni aliyehoji kuwa,

Kwakuwa takwimu zinaonyesha zinaonyesha kwamba kila watoto wanaozaliwa watoto wanne sio wa baba muhusika, Je? Serikali inaonaje juu ya udhalilishaji wa kina baba kwakubambikiziwa watoto ambao sio wa kwao kigenetic.

Si kweli kwamba watoto sita kati ya watoto wetu tuliokuwa nao sio wababa au wazazi husika naomba niweke vizuri takwimu ile na wale waliopeleka kupeleka vipimo vyao kwaajili ya vina saba kutambua uhalali wa mzazi, ni sawa sawa na unaenda katika wodi ya TB unataka kujua maambukizo ya wagonjwa wa TB katika wodi ya TB wale wote waliopeleka sample kwenye ofisi maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali ni wale wote wenye wasiwasi kuhusiana na uzazi wa wale watoto na ndio maana hicho kiwango kilichopatikana kikawa hicho,” amesema

Sio kwamba kwa ujumla wa Tanzania nzima hususa kwa kina baba watoto si wao sio kweli nilitaka niweke hiyo taarifa wazi ili wabunge especially wanaume tusianze kukimbia majukumu yetu ya msingi,” ameongeza.

Hata hivyo Naibu Spika, Tulia Ackson amesema kuwa “nilidhani wabunge wanawake wanataka kuandamana, Mh. Chegeni hilo swali lako na maelezo yako watu tuna watoto wengi humu ndani. Waheshimiwa wabunge Kiswahili cha kawaida kabisa kinasema kitanda hakizai haramu unaenda kupima wa nini.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents