Michezo

Andy Murray ajifua kufa kupona

Mchezaji tennis raia wa Uingereza, Andy Murray ameanza rasmi mazoezi katika kituo cha Patrick Mouratoglou academy huko nchini Ufaransa baada ya kupita takribani miezi mitatu tangu kufanyiwa upasuaji.

Bingwa huyo mara tatu wa taji la Grand Slam anatarajia kurejea uwanjani mwezi Juni mwaka huu lakini kunauwezekano mkubwa wa kurudi mapema zaidi ya inavyotarajiwa kufuatia mazoezi makali anayofanya.

Mwanachama mmoja wa kituo hicho ameiyambia AFP kuwa, Andy Murray amewasili usiku wa Ijumaa na kutarajiwa kuwa hapo hadi wiki ya kwanza ya mwezi Aprili.

https://www.instagram.com/p/BgwhDzhFs7I/?taken-by=taban069_tennis_club

Kipande kimoja cha video kimerushwa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram kikimwonyesha Murray akifanya mazoezi kwa juhudi kubwa kwenye kituo hicho akiwa na kocha wake, Jamie Delgado na mwalimu wake wa ‘fitness’, Matt Little na mtu wake wa saikolojia, Shane Annun.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents