Askari magereza watakiwa kuepuka rushwa

ASKARI Magereza nchini wametakiwa kudumisha nidhamu katika kazi ili kuwezesha utendaji wa kazi ulio bora, ikiwa ni pamoja na kuepukana na vitendo vya rushwa.

Gloria Tesha


ASKARI Magereza nchini wametakiwa kudumisha nidhamu katika kazi ili kuwezesha utendaji wa kazi ulio bora, ikiwa ni pamoja na kuepukana na vitendo vya rushwa.


Hayo yalisema juzi na Kamishna Mkuu wa Magereza, Augustino Nanyaro, alipokuwa akitoa salamu za mwaka mpya na kuuaga mwaka uliopita katika sherehe zilizofanyika katika ukumbi wa bwalo kuu la maofisa wa magereza Ukonga, Dar es Salaam.


Alisema nidhamu ndio msingi unaopaswa kuwa mstari wa mbele katika kuwezesha kufuata kanuni na sheria za kazi kwa makini ili kuwezesha kufuta minong’ono au lawama kwa jeshi hilo kwa wananchi.


“Ninapenda kuwashukuru wafanyakazi na kuwapa pongezi kwani kumekuwapo na mafanikio makubwa katika mwaka uliopita, licha ya kuwa na uhaba wa fedha na vitendea kazi ambavyo viliwaweka katika mazingira magumu na wakati mwingine kufuata kanuni za kazi, lakini sasa yameboreshwa na hivyo tufanye kazi kwa bidii mwaka huu,” alisema.


Kamishna mkuu huyo alisema kuwa hakuna ulazima ya kujisifia kwa kumaliza mwaka kama ni ushujaa wa mtu binafsi au ufundi si hivyo, bali ni bahati tu kwa hivyo aliwataka kuongeza juhudi na ushirikiano kazini kwa mwaka huu ili kupata mafanikio zaidi.


Katika sherehe hizo pia kulikuwa na zawadi mbalimbali ambazo zilitolewa kwa mfumo wa bahati nasibu kwa askari magereza ambazo ni friji, feni, vitambaa vya suti, vitenge na simu za mkononi, ikiwa ni motisha wa kufanyakazi kwa bidii na kuwajibika kwa masuala ya jeshi hilo. Nanyaro aliwataka waliopata vitu hivyo wasibweteke na waongeze bidii.


Source: Habari Leo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents